KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Mkuu wa polisi wa Afrika Kusini amelaani ufaytuliaji risasi kwa mtoto wa kiume wa umri wa miaka mitatu


Mauaji ya mtoto yaibua hasira A.Kusini

Mkuu wa polisi wa Afrika Kusini amelaani ufaytuliaji risasi kwa mtoto wa kiume wa umri wa miaka mitatu yaliyofanywa na ofisa wa polisi.
Bheki Cele ameyapuuza madai ya afisa huyo kwamba alifyatua risasi kujihami akiamini bomba alilokuwa ameshika mtoto huyo ni bunduki.

Ameiambia BBC kwamba mauaji hayo ni uhalifu wa kizembe akisema: "Hata kama ingekuwa bunduki ya kweli, usingeanza kufyatua risasi."

Lakini alitetea haki ya polisi kuweza kutumia nguvu inapobidi.

Atlegang Aphane alikuwa ndani ya gari ambalo polisi walidhani linaendeshwa na wanaoshukiwa kuwa wahalifu alipopigwa risasi siku ya Jumanne.

No comments:

Post a Comment