KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Maafa zaidi Afrika kutokana na saratani



Vifo kutokana na saratani vitaongezeka barani Afrika, ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Kulingana na wanasayansi wa Marekani, ongezeko hilo ni kutokana na sheria chache barani Afrika kuzuia uvutaji sigari wa kiholela.

Wanaovuta sigara wataongezeka maradufu katika kipindi cha miaka 12 ijayo, ikiwa mwenendo huu hautapunguza kasi, kulingana na shirika linalohusika na saratani nchini Marekani (American Cancer Society).

Ripoti ya shirika hilo inaelezea kwamba zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaoishi barani Afrika hawana kinga yoyote kutokana na moshi unaotoka kwa wavutaji sigara.

Baadhi ya mataifa ya Afrika yana sheria za kuzuia uvutaji sigara hadharani, lakini mataifa mengi bado hayana vikwazo vyovyote

No comments:

Post a Comment